Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa

Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa

You are Here: Home > News > Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa

Dar es salaam, Tanzania
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema mipango inayofanywa kwa ajili ya kusambaratisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kamwe haitafanikiwa.

Hayo aliyasema alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Makurumla, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo, ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Maalim Seif, alisema zimekuwa zikifanyika jitihada mbalimbali zenye mlengo wa kusambaratisha na ikiwezekana hata kuua Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), na alionye msimamo wake kwa kusema kuwa jitihada hizo mbovu zitakwama (hazitafanikiwa).

Maalim Seif Shariff Hamad

Maalim Seif Shariff Hamad!

“Umoja huu umeundwa kwa lengo la kutetea masilahi ya wananchi kupata Katiba wanayoitaka na wala siyo kwa masilahi binafsi... Nimefurahishwa na vyama vya upinzani kuunda umoja huu, kwani vinginevyo CCM ingewaburuza na kufanya uamuzi wanaoutaka kinyume na matakwa ya wananchi walio wengi,” alisema Hamad.

Tarehe 30 May mwaka huu (2014), Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani, walitoka nje ya ukumbi wa Bunge kususia kujadili makadirio ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini wakidai inakabiliwa na ufisadi mkubwa.

Kuhusu hilo, Maalim Seif alisema suluhisho pekee litakalowafanya wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani warejee Bungeni, ni pale Rais Jakaya Kikwete atakapowahakikishia kuwa rasimu itakayojadiliwa ni ile iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na iwapo itakwenda kinyume, kuna uwezekano mkubwa wa wao kutoka tena nje ya bunge hilo.

Kwa upande mwingine, Maalim Seif aliweka wazi msimamo wake kuhusu swala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kusema: njia pekee itakayomaliza kero za muungano ni kuruhusu muundo wa serikali tatu zitakazotoa mamlaka kamili kwa serikali za nchi washirika.

"......hata Katiba ikitoa mamlaka kwa Zanzibar kuhusu kuweza kujiunga na mashirika ya Kimataifa yakiwamo; Afya (Who), Chakula (Fao) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mamlaka hayo hayatokuwa na nguvu kwani mashirika hayo yanahitaji kufanya ushirikiano na nchi zenye mamlaka kamili (sovereign states)....." Alisema.

You may also like this!

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema...

Wabunge wa upinzani wasusia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini
Uhitimishaji wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini jana jioni ulizua tafrani kubwa bungeni, baada ya...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Wilaya ya Nzega
Wilaya ya Nzega ni miongoni mwa wilaya zinazounda mkoa wa Tabora, hapa Tanzania. Wilaya hii iko upande wa...

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi
Profesa Peter Mutharika aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu nchini Malawi kupitia chama cha...

Mwimbaji wa gospel kutoka Zanzibar, Stephano, amezungumza na mjknetten
Kijana Stephano Atilio Mwinyi, mwimbaji wa nyimbo za injili anayeishi Zanzibar kwa sasa, ni miongoni mwa watumishi wa...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment