Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili

You are Here: Home > News > Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili

Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema yupo karibu kukamilisha utengenezaji wa albamu yake ya pili.

Hayo aliyasema leo alipofanya mahojiano ya moja kwa moja na kitengo cha vyanzo vya habari cha blog hii kinachofahamika kama mjknetten spotter, kilipomtembelea nyumbani kwake maeneo ya Masingini, mji Unguja, Zanzibar.

Mrs Juvenalister Sylvester Mabumba akiwa binti zake Maryprisca na Catherine katika moja ya video za kwenye albamu yake ya kwanza

Juvenalister alizungumza mengi yanayohusu muziki wa injili, na sehemu kubwa ya mazungumza ilijikita katika uandaaji wa albamu yake ya pili anayotarajia kuizindua ndani ya mwaka huu.

Audio ya Albamu yake ya kwanza iliandaliwa katika studio za Fabric Studio zilizopo maeneo ya mbagala na Video yake ilitengenezwa katika studio ya ITC production ya jijini Dar Es Salaam na alifanikiwa kuizindua mnamo mwaka 2012. Albamu hiyo inaitwa Umeamua Vyema, ambalo ni jina la moja kati ya nyimbo zinazounda albamu hiyo.

Nyimbo zilizomo kwenye albamu yake ya kwanza ni:

  1. Ninakushukuru Mungu
  2. Harusi
  3. Umeamua Vyema
  4. Maafa / ajali ya Zanzibar
  5. Tutaimba Haleluya
  6. Yote unayopata
  7. Pokea sifa
  8. Yatima

Kwa mujibu wa maelezo ya Juvenalister ni kwamba nyimbo hizo zilisambazwa katika vituo mbalimbali vya redio hususani Wapo Redio, Press Power, Redio Maria na Upendo Radio. Kwa upande wa televisheni alisema alipeleka nyimbo moja (Umeamua Vyema) EATV (East Africa Television) na kuongeza kuwa huwa inachezwa mara kwa mara.

Akizungumzia albamu yake ya pili ambayo alisema itakuwa na jumla ya nyimbo nane, Juvenalister ambaye pia ana fahamika kama Mama Mabumba, alisema nyimbo sita (6) tayari zimeshatengenezewa audio. "Mpaka sasa nimesharekodi nyimbo sita ambapo nne kati ya hizo nimefanyia Makonelah Records na mbili nimefanyia Islands Records."

Kwa upande mwingine, ujio wa albamu hii unaonekana kuwa wa kishindo kikubwa hasa kutokana na ukweli kwamba Juvenalister amemshirikisha binti yake wa mwisho kuzaa anayefahamika kwa jina la Maryprisca. Maryprisca, ambaye yupo darasa la tatu katika shule ya Saint Monica iliyopo mjini Unguja, ameimba vizuri sana na kuweza kuzitendea vyema nafasi alizopewa kuimba.

"Safari hii nimeona niwaletee vionjo vipya na vya kipekee mashabiki wangu na wadau wa injili kwa ujumla na watumishi wote wa bwana kwa ujumla. Mwanangu anasoma darasa la tatu pale Saint Monica na anapenda kuimba. Kwa bahati nzuri bwana amemjalia sauti nzuri ya uimbaji na kikubwa zaidi ni kwamba ana uwezo mkubwa wa kuimba na anajiamini." Alisema Mama Juvenalister.

Aidha, mama Mambumba alisema hana msimamizi na msambazaji wa kazi zake. Kwa hiyo yeyote ambaye yupo tayari kumsaidia Mama Mabumba kusimamia kazi zake anaweza kuwasiliana naye.

Wito wake kwa mashabiki wake ni kumpa ushirikiano na kupokea albamu yake anayotarajia kuizindua mwishoni mwa mwaka huu (2014). "Unajua sisi waimbaji wa nyimbo za injili tunafanya kwa ajili ya kufikisha neno la MUNGU kwa watu wake. Kwa hiyo tunahitaji ushirikiano wa hali ya juu ili tuweze kuendelea kuwasilisha vyema kile ambacho baba ameagiza tukifanye kwa ajili ya jamii. Alimalizia Juvenalister.

You may also like this!

Wabunge wa upinzani wasusia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini
Uhitimishaji wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini jana jioni ulizua tafrani kubwa bungeni, baada ya...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi
Profesa Peter Mutharika aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu nchini Malawi kupitia chama cha...

Mwimbaji wa gospel kutoka Zanzibar, Stephano, amezungumza na mjknetten
Kijana Stephano Atilio Mwinyi, mwimbaji wa nyimbo za injili anayeishi Zanzibar kwa sasa, ni miongoni mwa watumishi wa...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment