Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Mwimbaji wa gospel kutoka Zanzibar, Stephano, amezungumza na mjknetten

Mwimbaji wa gospel kutoka Zanzibar, Stephano, amezungumza na mjknetten

You are Here: Home > News > Mwimbaji wa gospel kutoka Zanzibar, Stephano, amezungumza na...

MUNGU humpa kila mja wake uwezo wa kipekee katika kuhakikisha neno lake linawafikia walengwa. Kuna watu wengi sana ambao MUNGU amewapa uwezo wa kusema, kusikika na kusikilizwa na watu kwa ajili yake na kila mmoja utakuta anafikisha ujumbe kwa njia na mbinu tofauti tofauti.

Kijana Stephano Atilio Mwinyi, mwimbaji wa nyimbo za injili anayeishi Zanzibar kwa sasa, ni miongoni wa watumishi wa bwana ambao wameamua kufanya muziki huo kwa ajili ya kufikisha neno la MUNGU kwa jamii. Pia ni mwimbaji binafsi, kwa maana ya kwamba hayupo katika kundi la kwaya.

Akitokea nyanda za juu kusini mkoani Iringa, Stephano alianza kuimba nyimbo za Gospel mwaka 2008 akiwa Songea vijijini katika kijiji cha Luhimba. Kipaji chake cha uimbaji kilionekana na kuzidi kukua alipojiunga na kuanza kuumini katika kanisa la IAGT lililopo katika kijiji hicho cha Luhimba.

Akiwa katika kanisa hilo aliweza kujiunga na kwaya ya hapo kanisani, na baadae akaanza kufundisha kwaya hapo hapo kanisani.

Mara nyingi nilikuwa ninakutana naye katika studio za makonelah records zilizopo mjini Unguja, Zanzibar bila kuzungumza chochote zaidi ya salamu, kwa hiyo leo niliamua kumuita na kuongea naye kidogo katika mjknetten spotter ili niweze kuyafahamu japo kwa uchache yale yanayomhusu yeye na muziki wa injili kwa ujumla.

Stephano Atilio Mwinyi katika moja ya video zake

Akizungumzia historia yake kimuziki, Stephano alisema mara ya kwanza kurekodi nyimbo studio ilikuwa 2012, ambapo alifanikiwa kurekodi nyimbo ya kwanza kabisa na ambayo kwa mujibu wa maelezo yake binafsi, ni kwamba itabeba jina la albamu. Nyimbo hiyo inaitwa 'Ninao ushuhuda'.

"Nyimbo hii niliitengenezea Makonelah Records, chini ya Producer mkuu, Mr. Mussa Makonelah. Ni miongoni mwa nyimbo zangu nane zitakazokuwemo kwenye albamu yangu ya kwanza ambayo ninatarajia kuizindua mwanzoni mwa mwezi wa nane (August) Mwaka huu." Alisema Stephano.

Nilipomuuliza kwanini ameamua kuupa wimbo huo jina hilo (Ninao ushuhuda), alisema ndani ya moyo wake ana neno la mungu ambalo anatakiwa kulishuhudia kupitia uimbaji wa nyimbo za injili, na akaenda mbali zaidi kwa kusema, wimbo huo unamkumbusha mtu yeyote amtumainiye Bwana, amshuhudie ndugu yake na rafiki ama jamaa yake.

Kwa upande mwingine, Stephano alisema albamu yake ya kwanza itakuwa na jumla ya nyimbo nane kama zilivyoorodheshwa hapo chini:

  1. Ninao Ushuhuda (Itakayobeba jina la Albamu yake ya kwanza)
  2. Dozi ya magonjwa
  3. Kesheni mkiomba
  4. Bwana waone
  5. Neno la Mungu
  6. Message sent
  7. Nikikumbuka
  8. Nagonga hodi

Nyimbo zote zilitengenezwa katika studio ya Makonelah Records isipokuwa moja inayoitwa Nagonga hodi ambayo kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Stephano ni kwamba ilitengenezwa katika studio ya SB production ya jijini Dar Es Salaam.

Alishawahi kusambaza Audio ya nyimbo hizo katika vituo mbalimbali vya redio kama vile, Ebony FM, Upendo Radio, Furaha, n.k.

Kwa upande wa video, Stephano alisema anamshukuru MUNGU kwa kuwezesha kuanza vizuri kwa zowezi la uandaaji wa Video kwa nyimbo zote na mpaka muda huu ameshakamilisha utengenezaji wa video za nyimbo mbili. Zoezi la utengenezaji wa video linafanyika Makonelah Records Video Production.

Pia, akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo hawa watumishi wa MUNGU hapa Zanzibar, alisema changamoto kubwa zipo katika usimamizi na utangazaji wa kazi zao. "Changamoto zipo nyingi, lakini zile ambazo mimi binafsi naziona kuwa ni sugu, ni pamoja na ukosefu wa ma-promota (watangazaji) na wasambazaji wa kutosha kwa ajili ya kutusaidia kutangaza na kusimamia kazi zetu.

Changamoto nyingine ni uhaba wa ma-prodyuza (watengenezaji) na studio zinazotengeneza muziki wa injili kwa hapa Zanzibar pamoja na waimbaji binafsi kusahaulika na kutokushirikishwa katika matukio muhumu yanayofanyika makanisani."

Kwa upande mwingine, Bw. Stephano amewashukuru na kuwapongeza waimbaji na wadau wote wa muziki wa injili hapa Zanzibar kwa kudumisha mshikamano na ushirikiano wa hali ya juu.

Shukrani zake za dhati kabisa hakusita kuzitoa kwa watu waliomuwezesha kufika hapo alipo kwa namna moja ama nyingine:

  1. Michael Sunday (Mwalimu wa kwaya Matendo - Dar Es Salaam)
  2. Dada Flowrance (Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Zanzibar)
  3. Joseph Gabriel Marwa (MCH. TAG Mbweni, Zanzibar)
  4. Nassor Khamis Mohammed (Bosi wake kazini, Zanzibar)

Mwisho kabisa Stephano amewaomba watu wazipende na kuzisapoti kazi za MUNGU wanazozifanya waimbaji wa injili. "Watu wasapoti na kutoa ushirikiano katika kazi tunazozifanya waimabji wa injili, kwa sababu sisi ni wawakilishi wa BWANA, tunatangaza neno la MUNGU, na tuna hakikisha kila mtu anajiweka katika mikono safi na salama ya Yesu kristo - Amen!" Alimalizia Stephano.

Mjknetten Blog inamtakia kila la kheir Stephano pamoja na waimbaji wengine ambao wanafanya kila waliwezalo ili kufikisha neno la MUNGU mahala linapotakiwa kufika.

You may also like this!

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema...

Wabunge wa upinzani wasusia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini
Uhitimishaji wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini jana jioni ulizua tafrani kubwa bungeni, baada ya...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi
Profesa Peter Mutharika aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu nchini Malawi kupitia chama cha...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment