You are Here: Home > News > Wabunge wa upinzani wasusia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani wakitoka nje ya bunge! Uhitimishaji wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini jana jioni ulizua tafrani kubwa bungeni, baada ya wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani kutoke nje ya ukumbi wa bunge. Habari zinasema kuwa wabunge hao waliamua kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mikakati waliojiwekea wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ya kufukia kashfa ya IPTL inayoikabili Wizara ya Nishati na Madini. Akitoa sababu zilizopelekea wabunge hao kutoka nje, Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani, Bw. Freeman Mbowe, alisema hawakuweza kuendelea na mjadala kutokana na kupingwa kwa hoja zao na kuzomewa na wabunge wa chama tawala, CCM. “Mheshimiwa Spika, nashawishika kabisa kusema kuendelea kushiriki mjadala huu ni sawa na kutowatendea haki wananchi wetu, sina matatizo na Waziri Muhongo, wala katibu wake, tatizo langu ni mfumo. Waheshimiwa wabunge, hebu someni hotuba yetu mjue tunasema nini. “Watu hamsomi, hamfanyi utafiti, lakini mmeshaweka misimamo kwa kutumia uwingi wenu, hatuwezi kushiriki mjadala kama huu tunapoona mambo yanachakachuliwa waziwazi, kuendelea kushiriki mjadala huu ni kulinajisi taifa, ni bora tuwaachie mjadala huu muhitimishe nia yenu kwa raha,” Hiyo ni kauli ya Mbowe aliyoitoa kabla hawajatoka katika ukumbi wa bunge. Aidha, Mbowe alisema alivunjwa moyo na kitendo cha kuwataka wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kutoa ushahidi papo hapo kila walipojaribu kuibua hoja ya kashfa ya IPTL bila kuwapa muda wa kutosha kwa lengo la kuwatisha, na kwamba wabunge wa CCM walipanga kukataa hoja ya kutaka iundwe Kamati Teule kuchunguza kashfa hiyo. Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani walioombwa kutoa ushahidi ni pamoja na John Mnyika na David Kafulila. Pia, CCM kukalia ripoti mbalimbali, kama vile ripoti ya maazimio ya kashfa za Richmond, uchunguzi wa vurugu za Mtwara pamoja na ripoti ya Jairo, ni sababu nyingine zilizowafanya wabunge hao kutoka nje. Mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, waziri mkuu, Mizengo Pinda alitoa kauli yake akionyesha wazi kukerwa na kitendo walichokifanya wabunge wa kambi ya upinzani. "....haiwezekani kila unapowasilisha hoja na ukiona inashindwa, njia rahisi iwe kutoka nje ya bunge.......si jambo zuri kwa viongozi kama hao kutoka, tunabishana hapa kwa hoja. Sasa kama umeleta hoja, unajenga hoja, haina sababu ya kutoka nje ya bunge...." Hayo ni maneno yake waziri mkuu, Mizengo Pinda. You may also like this!
Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Berry Black kupakua ngoma mpya makonelah records
Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa!
Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi |
Internet basics tutorials! Learn the Internet basics on our free Internet tutorials. Learn how to surf the web and a variety of other related matters we offer on this blog. Get started now! Advertisement! Blogging tips and tutorials! Learn what the blog is, its importance, how to create it and other related topics in our free blogging tutorials! About this blog's Author!
Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as..... Advertisement! |
No comments:
Post a Comment