Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Berry Black almaarufu Mfalme wa Zenji Fleva, amerekodi ngoma mpya katika studio za Makonelah Records mjini Unguja. Berry Black ameamua kumshirikisha msanii mwenzake, Samir katika nyimbo hiyo ambayo taarifa zinasema kuwa ataitoa muda wowote kwa mashabiki wake, utengenezaji wake ukishakamilika. Kama nilivyosema hapo juu, ni kwamba ngoma hiyo inatengenezewa katika studio za Makonelah Records zilizopo mjini unguja (Zanzabr). Naimani mashabiki wa Berry Black mtafurahi kwa ujio wa ngoma hiyo, kutokana na ukweli kwamba Berry amekuwa akijitahidi kushirikisha wasanii wenzake, kitu ambacho kinafanya nyimbo zake ziwe na ladha tofauti-tofauti, na kuleta burudani murua kwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya. Aidha, nikizungumza na mmiliki, mwendeshaji na pia producer mkuu wa studio za Makonelah Records Bw. Musa Makonelah, aliniambia kuwa nyimbo hiyo anaifanyia 'Mixing' (Anaiweka katika hali sawa ili ikae mkao wa kinyimbo kamili na yenye kusikilizika), na kwamba akishamaliza majukumu yake katika nyimbo hiyo kama producer, ataikabidhi kwa Berry ili iweze kuingia sokoni. Kila la kheri Berry Black! Makonelah records ni miongoni mwa studio kongwe za muziki visiwani Zanzibar zinazofanya vizuri kunako 'Game' la muziki wa kizazi kipya nchini. Ipo maeneo ya Mchina Mwanzo, ikiongozwa na Mr. Musa Makonelah. Kwa taarifa zaidi unaweza kuwatafuta kupitia tovuti yao ya http://makonelahrecordz.blogspot.com/ Picha ya Msanii Berry Black You may also like this!
R. One wa Keroh apania kurudi tena kwenye gemu la muziki wa bongo flava
Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa! |
Internet basics tutorials! Learn the Internet basics on our free Internet tutorials. Learn how to surf the web and a variety of other related matters we offer on this blog. Get started now! Advertisement! Blogging tips and tutorials! Learn what the blog is, its importance, how to create it and other related topics in our free blogging tutorials! About this blog's Author!
Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as..... Advertisement! |