Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Wanajeshi 17 wauawa mpakani Iran

Wanajeshi 17 wauawa mpakani Iran

You are Here: Home > News > Wanajeshi 17 wauawa mpakani Iran

Imeripotiwa kuwa walinzi wa mpaka kati ya Pakistan na Iran wapatao 17 wameuawa na wengine saba kujeruhiwa, katika mapambano yaliyokuwa yakifanyika kati yao na watu waliokuwa na silaha.

Taarifa hizi zimetolewa na Shirika la habari la Iran (IRNA). Tukio hilo la kutisha limetokea mpakani mwa nchi hizo mbili, Iran na Pakistan kwenye eneo la milima nje ya mji ujulikanao kwa jina la Saravan, katika jimbo la Baluchestan.

Inasemekana kuwa Washambuliaji hawajulikani, na habari kutoka kwa mjumbe mmoja wa bunge la Saravan, Hedayatollah Mirmoradzehi, amesema kwamba waliowashambulia walinzi hao ni magaidi wanaopinga mapinduzi.

Kwa upande mwingine, naibu waziri wa mambo ya ndani, Ali Abdollahi, aliliambia leo Jumamosi (october 26 2013) shirika la IRNA, kuwa maafisa wa mipaka wanafanya uchunguzi juu ya shambulizi hilo, na kuahidi kuwa matokeo ya uchunguzi yatatangazwa muda wowote.

Walinzi wa Iran wakilinda Mpakani kabla ya tukio

You may also like this!

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema...

Berry Black kupakua ngoma mpya makonelah records
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Berry Black almaarufu Mfalme wa Zenji Fleva, amerekodi ngoma mpya katika studio za...

Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa!
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema mipango inayofanywa...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Wilaya ya Nzega
Wilaya ya Nzega ni miongoni mwa wilaya zinazounda mkoa wa Tabora, hapa Tanzania. Wilaya hii iko upande wa...

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi
Profesa Peter Mutharika aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu nchini Malawi kupitia chama cha...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!