Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Wilaya ya Nzega

Wilaya ya Nzega

You are Here: Home > News > Wilaya ya Nzega

Wilaya ya Nzega ni miongoni mwa wilaya zinazounda mkoa wa Tabora, hapa Tanzania. Wilaya hii iko upande wa kaskazini mwa mkoa wa Tabora. Inapakana na mkoa wa Shinyanga kwa upande wa kaskazini, Wilaya ya Igunga kwa mashariki na Tabora manispaa kwa upande wa magharibi na kusini.

Ina Tarafa mbili, Bukene na Nyasa. Pia ina kata na vijiji vingi, k.v. Nata, Nyasa, Puge, Mwangoye, Iyuki, Mwaguguli, Itobo, mwamala, n.k. Ina majimbo mawili ya uchaguzi, ambayo ni Nzega mini na Bukene. Mbunge wa sasa(2010-2015) katika jimbo la Nzega ni Dr.Hamis Andrea Kingwangallah.

Wilaya hii ni miongoni mwa sehemu za Tanzania zenye maliasili za aina nyingi, ikiwa ni pamoja na misitu na madini ya Dhahabu. Sehemu maarufu kwa uchimbaji wa Dhahabu ni Isanga na Isungangwanda.

Wananchi wa maeneo haya wanajishughulisha na kilimo, ufugaji wa wanyama (ng’ombe, mbuzi, kondoo, n.k.), na biashara za aina mbalimbali. Pia kuna wengine wameajiliwa, serikalini au katika makampuni binafsi katika nyadhifa mbalimbali. Biashara kuu maeneo hayo ni ya mpunga, mahindi, pamba, alizeti na maduka yanayouza bidhaa za aina mbalimbali.

Mitaa maarufu mjkini Nzega ni pamoja na Uzunguni, Kitongo (A & B), Nyasa, Maporomoko, Majengo, Majarubani, Uchama, Kashishi (Airport), Ushirika n.k.

Maeneo mengine yaliyoko nje ya mji ambayo yanakuja juu kwa kasi kiuchumi ni Bukene, Itobo, Mwamala, Nata, Puge, Nzega Ndogo, n.k.

Katika suala la elimu, wilaya hii imejitahidi kwa kiwango kikubwa na bado jitihada zinafanywa na serikali na mashirika au watu binafsi katika kuhakikisha kuwa wilaya ya Nzega inapanda chati kielimu. Shule za sekondari na msingi zimeongezeka vya kutosha, na hivyo kutoa nafasi kwa watoto wengi kupata elimu. Baadhi ya shule za sekondari katika wilaya hii ni, Nata, Uchama, Bulunde, Itobo, Mwangoye, Badri, Chief Ntinginya, Nzega Day, n.k. Pia kuna vyuo Viwili; kimoja cha VETA, kipo mjini maeneo ya Kitongo na cha walimu kilichopo maeneo ya Ndala, nje ya mji wa Nzega.

Changamoto zilizopo katika wilaya hii ni pamoja na:-

  1. Barabara nyingi ni za vumbi mjini
  2. Usafiri kwenda maeneo ya vijijini ni wa taabu (hakuna daladala, kuna ‘Ganagana’ tu na Bodaboda)
  3. Hakuna maji safi vijijini, na kwa mjini hayatoshi
  4. Nauli kubwa katika usafiri wa daladala (hatua kadhaa unatoa shilingi elfu mbili...au elfu)
  5. Hakuna daladala zinazozunguka mjini (labda ukodi)
  6. Hakuna Umeme hata katika sehemu (vijiji au kata) zinazoendelea, kama vile Mwangoye, Itobo na Mwamala.
  7. Hakuna vyuo vikubwa vya elimu (mwanafunzi wa kidato cha sita akifaulu lazima aende nje ya wilaya, na anaye feli hawezi kujiendeleza kielimu wilayani humo) ukiachilia chuo cha VETA.

Je, wewe unaifahamu Nzega pamoja na vitongoji vyake kwa undani, na uko tayari kuchangia chochote kuhusu nilichokiandika?............ Feel free! Jiachie hapo chini, Iwe kwa Facebook, Twitter, kwa E-mail yetu au njia yoyote ambayo unafikiri itafikisha ujumbe.

Thanks!

Picha ya Nzega mjini!

You may also like this!

Wanajeshi 17 wauawa mpakani Iran
Imeripotiwa kuwa walinzi wa mpaka kati ya Pakistan na Iran wapatao 17 wameuawa na wengine saba kujeruhiwa, katika...

Berry Black kupakua ngoma mpya makonelah records
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Berry Black almaarufu Mfalme wa Zenji Fleva, amerekodi ngoma mpya katika studio za...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!