Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi

You are Here: Home > News > Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi

Lilongwe, Malawi
Profesa Peter Mutharika aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu nchini Malawi kupitia chama cha Democratic Progressive Party (DPP), ametangazwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo.

Tume ya Uchaguzi nchini humo, MEC iliamua kutangaza matokeo hayo Ijumaa ya tarehe 30 usiku baada ya kutokea mvutano mkali baina ya tume hiyo na mgombea Banda, aliyekuwa akishinikiza kutokutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20, Mei mwaka huu, kulitokea mtafaruku mkubwa ambapo mgombea wa urais, Joyce Banda alitangaza kufuta uchaguzi huo kwa kudai ulijawa na vitendo vya wizi wa kura pamoja na kukiukwa kwa taratibu nyingine za kuhesabu kura.

Rais Mutharika akifurahi pamoja na wafuasi wake baada ya kuapishwa!

Rais Mutharika akifurahi pamoja na wafuasi wake baada ya kuapishwa!

Profesa Mutharika alitangazwa na MEC kuwa rais baada ya kuwashinda wagombea wengine 12 kwa tofauti ya asilimia 36.4. Wagombea wengine ni Lazarous Chakwera wa chama cha Malawi Congress Party (MCP), aliyepata asilimia 27.8, Joyce Banda asilimia 20.2 na Atupele Muluzi wa chama cha UDF aliye shika nafasi ya nne baada ya kujizolea asilimia 13.7.

Awali, baada ya kushindwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo, Banda alitangaza uchaguzi huo ungefanyika ndani ya siku 90 na aliahidi kutokugombea tena.

Watu waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa awamu hii walikuwa milioni 7.5 na waliopiga kura walikuwa milioni 5.3 sawa na asilimia 70.78 na kura zilizoharibiika ni 56,675.

Aidha, Mwenyekiti wa MEC, Jaji Maxon Mbendera, baada kumtangaza Prof. Peter Mutharika kuwa Rais wa Malawi, alizungumza mengi ambapo kubwa zaidi alimtaka Mutharika aendeshe serikali ya Malawi kwa umakini, uadilifu na uaminifu mkubwa bila kuwa na upendeleo wa aina yoyote.

Tume ya Uchaguzi nchini Malawi, MEC iliiomba Mahakama Kuu ya Malawi iongeze siku 30 ili itangaze matokeo baada ya kumaliza kurudia kuhesabu kura, lakini mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi hilo na kuagiza yatangazwe Ijumaa ya Tarehe 30 Mei, mwaka huu (2014).

You may also like this!

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema...

Wabunge wa upinzani wasusia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini
Uhitimishaji wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini jana jioni ulizua tafrani kubwa bungeni, baada ya...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Mwimbaji wa gospel kutoka Zanzibar, Stephano, amezungumza na mjknetten
Kijana Stephano Atilio Mwinyi, mwimbaji wa nyimbo za injili anayeishi Zanzibar kwa sasa, ni miongoni mwa watumishi wa...

R. One wa Keroh apania kurudi tena kwenye gemu la muziki wa bongo flava
Baada ya msanii wa bongo flavour Rashid A. Rashid a.k.a R. One wa Keroh, kukaa kimya kwa muda mrefu kimuziki, ameamua...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment