Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

R. One wa Keroh apania kurudi tena kwenye gemu la muziki wa bongo flava

R. One wa Keroh apania kurudi tena kwenye gemu la muziki wa bongo flava

You are Here: Home > News > R. One wa Keroh apania kurudi tena kwenye gemu la muziki wa bongo

Baada ya msanii wa bongo flavour Rashid A. Rashid a.k.a R. One wa Keroh, kukaa kimya kwa muda mrefu kimuziki, ameamua kurudi tena kwa kasi ya ajabu, akiwa amejipanga kufanya mambo makubwa katika muziki wa kizazi kipya. Haya ameyazungumza leo (23/05/2014) katika mahojiano ya LIVE tuliyoyaendesha kwa takribani masaa mawili katika studio za muziki za Makonelah Records, mjini Unguja.

R. One ni miongoni mwa wasnii wanaowakilisha Zanzibar katika Muziki wa Bongo Flavour, na ana muda mrefu tangu aingie katika fani ya muziki. Alianza kuimba akiwa jijini Dar essalaam, na nyota yake ya muziki iling'ara baada ya kuhamia katika visiwa vya marashi, Zanzibar.

Picha ya kushoto ni R. One wa Keroh na producer Buju wakiwa makonelah Records, ya kulia ni R. One akiingiza Vocal (sauti) katika studio za makonelah Records!

Nyimbo iliyomtambulisha R. One kunako 'game' na kumpatia umaarufu inaitwa 'My wife ambayo aliitengeneza na kuitoa mnamo 2010, akimshirikisha mwanadada Suz. Nyimbo hii ilimuwezesha kufanya SHOW mbalimbali, za ndani na hata nje ya Zanzibar. Nyimbo yake iliweza kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio, vya hapa Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Nyimbo hii ilitengenezwa katika studio za Makonelah Records na producer Makonelah na msaidizi wake Chief Elia.

Mnamo mwaka 2012 Wa Keroh akatoa Ngoma nyingine inayoitwa Jipange akimshirikisha msanii anayefahamika kwa jina la Juma Black. Baada ya kutoa nyimbo hiyo alikaa kimya (bila kutoa ngoma wala kusikika akizungumzia muziki katika vyombo vya habari) hadi leo hii ambapo ameamua kurudi tena akiahidi kufanya mapinduzi makubwa zaidi katika muziki wa Kizazi kipya.

Katika Exclusive Interview niliyoifanya leo na msanii huyu, nilimuuliza amejipanga vipi kuhakikisha ujio wake unapokelewa kwa shangwe na vifijo kutoka kwa mashabiki, akanijibu bila kung'ata mdomo: "Mi nimejipanga vizuri, vya kutosha, kistaili ya uimbaji, kiujumbe, nina Idea tofauti-tofauti na kikubwa zaidi ni kwamba nina project ambayo nitaikamilisha hivi karibuni...." Aliema wa Keroh!

R. One alisema ana projetct ya kutengeneza Ngoma moja katika studio za Makonelah Records ikisimamiwa na maprodyuza wawili, Makonelah (wa makonelah Records) na producer Buju (wa Mandevu Records). Ngoma hiyo ameipa jina la Gari haifiki. Ngoma ilisharekodiwa, kinachofanyika sasa hivi ni umaliziaji (Mixing) tu na baada ya hapo itatolewa rasmi na kuanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio.

Nilipomuuliza sababu iliyopelekea nyimbo hiyo aamue kuipa jina hilo, R. One alisema inazungumzia maisha halisi ya uswahilini ambako miundombinu kama vile barabara, haishughulikiwi, jambo ambalo linasababisha vyombo vya usafiri vishindwe kufika au vifike lakini kwa taabu. "Unajua nyumba za Uswahilini zimejengwa kwa kubananishwa bila kufuata taratibu za Mipango Miji, kwa hiyo njia za kupita gari hakuna, au zinaweza kuwepo lakini utakuta zina mabonde, maji au matope kiasi kwamba gari haiwezi kupita." Alisema R. One.

Kwa ufupi ni kwamba nyimbo hii inazungumzia mapenzi kati ya R. One akiishi Uswahilini na mwanamke ambaye anakaa mitaa ya wakubwa (!?!?). Wa keroh anamwaita mwanamke uswahilini (kwa R. One) lakini asipande gari kwa sababu gari haiwezi kufika nyumbani kwa R. One. Pia nyimbo hii imezungumzia upatikanaji wa vyakula vya asili katika maeneo ya uswahilini. Nyimbo imezungumzia vitu vingi na siwezi kuvitaja vyote, lakini ikitoka nitafanya utaratibu wa kui-post katika blog hii ya mjknetten (kwa kutegemea idhini yake) ili kila mmoja afaidi ujio wa kijana huyu!

R. One ameshafanya shoo nyingi sana hapa Zanzibar, Dar essalaam pamoja na mikoani pia. Amewahi kushirikishwa na wasanii wengi wanaofanya muziki wa bongo flavour, kama vile BND katika nyimbo ya Njoo mummy. Pia amewahi kushirikishwa na kundi la Wamanzese pamoja na Vasapo.

R. One amewaomba mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hapa nyumbani (BONGO) wampe sapoti na ushirikiano wa hali na mali ili aweze kuuwakilisha muziki wa bongo flava kitaifa na kimataifa. "Bila nguvu ya mashabiki siwezi kufika popote, kwa hiyo nahitaji sana ushirikiano wenu... Nina muda wa kutosha wa kufanya muziki kwa utulivu, na kwa muda mrefu niliokaa kimya kuna mengi nimejifunza, kwa hiyo nitayachukulia kama changamoto kwa ajili ya kufanya mazuri niwafurahishe fans wangu. Nawapenda sana!" Anamalizia R. One wa Keroh!

Mtafute R. One Kwenye Facebook kwa taarifa zaid!

You may also like this!

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema...

Berry Black kupakua ngoma mpya makonelah records
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Berry Black almaarufu Mfalme wa Zenji Fleva, amerekodi ngoma mpya katika studio za...

Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa!
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema mipango inayofanywa...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment