Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club kuamua hatima ya wagombea wenye dosari kesho

Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club kuamua hatima ya wagombea wenye dosari kesho

You are Here: Home > News > Kamati ya uchaguzi ya Simba Sports Club kuamua hatima ya...

Kesho, tarehe 25/05/2014 ni siku ambayo wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba SC ya jijini Dar essalaam, wanaingojea kwa hamu kubwa. Hii inatokana na taarifa iliyotolewa leo na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa timu hiyo, Mwanasheria na wakala wa wachezaji wa FIFA, Dr. Damas Daniel Ndumbaro, kwamba kesho kamati itakaa kusikiliza mapingamizi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika timu hiyo.

Picha ya kushoto ni nembo ya club ya Simba SC. Ya kulia ni ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa timu ya simba, Mwanasheria na wakala wa wachezaji wa FIFA, Dr. Damas Daniel Ndumbaro

Zoezi hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa tatu kamili asubuhi katika ukumbi wa Gymkhana jijini Dar es salaam, ambapo Ndumbaro amesema zoezi hilo litazingatia haki kwa sababu kamati yake inajumuisha watu makini na wenye malengo ya kuipatia Simba sc viongozi bora watakaoiwezesha timu ya Simba SC kufanikiwa.

Ndumbaro alisema lengo lao si kuwaondoa wagombea bali, bali kanuni za uchaguzi za TFF na katiba ya Simba ndizo zitakazopelekea wagombea hao kuondolewa. “Msimamo wetu uko pale pale, sisi hatumuondoi mgombea, bali kanuni za uchaguzi za TFF na katiba ya Simba ndizo zitakazomuondoa mgombea”. Alisema Ndumbaro.

Aidha, Dr. Ndumbaro alisema watu wote waliowawekea pingamizi wagombea, wanapaswa kufika muda mwafaka wakiwa na viambatanisho vyote, na akaongezea kwa kusema kwamba yeyote atakayeshindwa kuhudhuria, pingamizi lake halitasikilizwa.

Kwa upande mwingine, hali ni tete kwa wagombea ambao inasemekana wana kasoro za hapa na pale. Mmoja wapo wa wagombea hao ni Michael Wambura, amabye ana kosa la kukiuka vifungu vya katiba ya Simba na ya TFF, vinavyoamuru kufungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa mwanachama au kiongozi yeyote anayehusisha mahakama za kiraia kwenye maswala ya soka.

wagombea wengine wenye dosari ni wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais Joseph Itang’are almaarufu 'Kinesi', aliyekuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumsimamisha Rage na Swedi Nkwabi aliyepachikwa cheo cha Makamu Mwenyekiti baada ya mapinduzi pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Ibrahim Masoud 'Maestro' anayewania pia nafasi hiyo.

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment