Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Frank Lampard yuko mbioni kuiacha Chelsea

Frank Lampard yuko mbioni kuiacha Chelsea

You are Here: Home > News > Frank Lampard yuko mbioni kuiacha Chelsea

London, England
Mshambuliaji mahiri anayeitumikia Club ya Chelsea FC ya nchini Uingereza, Frank Lampard, anatarajia kuiacha Club hiyo maarufu katika ulimwengu wa soka.

Habari zinadai Lampard anaondoka klabuni hapo ktokana na kushindwa kuwa na mwafaka mzuri juu ya mkataba mpya.

Lampard (35), anaondoka Klabuni hapo baada ya mkataba wake kuisha, ambapo taarifa zinasema mwishoni mwa mwezi huu (Juni) utakuwa mwisho wa kuitumikia klabu hiyo yenye mashabiki lukuki duniani.

Mchezaji huyo alijiunga Chelsea akitokea West Ham United, manamo 2001, ameitumikia klabu ya Chelsea kwa misimu 13, akifunga mabao 211, kitendo kinachompa nafasi ya kuwa na rekodi ya kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo.

Mchezaji Frank Lampard Akiwa Chelsea FC

Mchezaji Frank Lampard Akiwa Chelsea FC!

Chelsea ilimsajili kwa pauni milioni 11, ambapo mpaka sasa ameshacheza mechi 648, akiwa mchezaji wa tatu kwa kucheza mechi nyingi zaidi, kwa kutanguliwa na Ron Harris (aliyecheza mechi 795) na Peter Bonetti (aliyecheza mechi 729).

Aidha, Lampard si mchezaji pekee kuondoka Stamford Bridge msimu huu, kwani hata beki wa kushoto, Ashley Cole (33) aliyecheza hapo kwa miaka minane, hatokuwepo.

Hata hivyo, pamekuwapo na taarifa zinazodai kuwa Lampard atakwenda Marekani kuchezea klabu flani kubwa ya huko wakati klabu nyingine zaidi ya 15 zinamtaka.

Kwa upande mwingine, Chelsea imemshukuru Lampard na kumtakia kila la kheri katika maisha yake atakayoishi baada ya kuondoka klabuni hapo.

"Lampard bado hajasema wapi atakwenda, lakini sisi kama Chelsea tunamtakia kila la kheri katika maisha yake. Anaondoka na shukrani zetu kubwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya miaka 13....." Ripoti kutoka klabuni.

Naye Lampard 'bila kumeza maneno' alielezea mafanikio aliyoyapata wakati akiitumikia timu hiyo!

"Nilifika katika klabu hii ya 'ajabu' miaka 13 iliyopita sikuamini kama ningekuwa na bahati ya kucheza mechi nyingi, kitu ambacho kimetoa mafanikio kwangu pamoja na timu yangu. Klabu hii imekuwa sehemu ya maisha yangu na kuna watu wengi ninaopaswa kuwashukuru kwa nafasi hii. Kwanza kabisa namshukuru Ken Bates, ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha ninasaini mkataba nikiwa mchezaji mchanga." Alisema Frank Lampard.

Vyanzo vikuu vya taarifa hii!

Chelsea FC Official Website
http://www.dailymail.co.uk Website!

You may also like this:

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment