Facebook Fan Page Computer Tutorials News Blogging Internet Latest Posts

Today is:

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha

You are Here: Home > News > Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha

Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa tamko rasmi juu ya taarifa zinazozidi kuenea kwa kasi katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kwamba CCM wilayani Nzega inataka kumnyang'anya kadi ya uanachama.

Dr. Hamis Kigwangalla

kigwangalla ameweka wazi mambo manne:
Moja, amesema watu wasichukulie kuwa ameshindwa vita na 'mtu' yeyote katika juhudi anazozifanya kwa kuwa hakuwahi kupigana na mtu yeyote, bali na umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na umbumbumbu.

Pili amewambia watu waelewe kuwa hawezi kukata rufaa ya kunyang'anywa uanachama ama vyovyote vile kwa kuwa hakuingia kwenye siasa kutafuta ajira ama cheo cha kuwafurahisha wengine bali aliamua kutoa mchango wake kwa taifa (service to the nation) kupitia uwakilishi. Pia Dr. Hamis alisema wanaotaka kumshughulikia, wanapaswa kufuata kanuni na taratibu zilizoandikwa. "Huwezi kuniadhibu bila kunishtaki, na bila kunipa fursa ya kusikilizwa! Na huwezi kunihukumu kwa jambo ambalo lipo mahakamani na hukumu bado haijatoka!". Ndivyo alivyosema bwana Kigwangalla katika jambo la pili.

Tatu, amewaomba watu waelewe wazi kuwa mawazo ya kuanzisha benki, kuanzisha kampuni ya ujenzi (kuchimba visima na kuchonga mabarabara) si yake peke yake, bali ni maazimio ya vikao vingi ambapo walipewa ushauri wa kitaalamu, wakaona inawezekana na ni miradi endelevu na yenye tija, na yeye ndiye aliyekuja na wazo la awali. Na hapa anazungumza, "hoja yangu ni kwamba kama wenzangu wanataka kubadilisha matumizi ya pesa hizi, walete hoja ya kufuta azimio la awali kwa mujibu wa utaratibu wa Kanuni zetu za kudumu za Halmashauri na si kupitisha azimio jingine juu ya azimio la zamani (ambalo liliishaanza kufanya kazi kwa madiwani kwenda semina). Utaratibu wa kugawa pesa kwa usawa kwenye Kata haupo, na hata kama watabadilisha matumizi basi wazipeleke kwenye miradi na madiwani wasihusike kuchagua nani apewe mradi. Miradi watakayoichagua ni lazima iwe endelevu, inayozalisha kipato na yenye taswira ya kuwa alama ya historia ya uwepo wa mgodi Nzega".

Nne, ameuambia umma uelewe kuwa hakuna mwenye uwezo wa kumnyang'anya heshima ya kuwa Mbunge wa kwanza kuanzisha hoja ya 'ushuru wa huduma' na akafanikisha miaka 15 toka kuingia kwa uwekezaji kwenye migodi mikubwa. Pia aliwataka wanaooonekana leo wanajua zaidi kupanga matumizi ya fedha wafanye jitihada za kuzichukua Tsh bilioni 4 ambazo bado hazijachukuliwa machimboni.

Ads

Aidha, Dr. Kigwangallah alisema, hatowasusia fisi bucha na kwamba ataendelea kuzuia pesa hizi zisiliwe mpaka wakubwa watakapoingilia kati. "Ninawaahidi walau moja kuwa 'sintowasusia fisi bucha', nitaendelea kuzuia pesa hizi zisiliwe mpaka wakubwa watakapoingilia kati na kuingiza hekima na busara kwenye vichwa vya wenzangu hawa. Nitaendelea kusimamia haki ya wananzega kwa kuzilinda pesa hizi kwa njia ya mahakama kama ambavyo nimefanya na kama ikishindikana kuelewana ni bora zisitumike mpaka tumalize muda wetu. Pengine msimamo huu utawafanya waelewe kuwa sifanyi haya kwa malengo ya kutafuta umaarufu wa kura za 2015, kwanza ni nani anayewadanganya kuwa nitagombea tena Ubunge wa Nzega mwaka 2015?"

Hii imekuja baada ya Dr. Kigwangalla kutoa taarifa kwa vyombo vya habari tarehe 24 mwezi january 2014, kuwa amekata tamaa na hawezi kuendelea kupambana na watu wanaotumia nafasi zao serikalini kukwamisha juhudi zake za kuleta maendeleo katika jimbo lake la Nzega. Taarifa za yeye kuonesha kukata tamaa ziliwavunja mioyo wengi hususani wanaomuunga mkono.

Chanzo kikuu cha haya yanayotokea Nzega ni pesa Tsh. Bil. 2 zilizopatikana katika mgodi wa Dhahabu wa Lusu, zilizopatikana baada ya Dr. Kigwangalla kufuatilia kwa muda mrefu. Pesa hizo ndizo zinaleta mvutano baina ya madiwani wanaotaka kila kata ipatiwe kiasi fulani cha pesa hizo, na upande wa pili ni wa mbunge (Kigwangalla) na raia wengine wa jimbo la Nzega ambao hawataki pesa hizo zitolewe kwa madiwani.

You may also like this!

Juvenalister yupo karibu kutoa albamu yake ya pili
Muimbaji wa muziki wa Gospel au nyimbo za injili kutoka Zanzibar, Mrs. Juvenalister Sylvester Mabumba amesema...

Maalim Seif amewatia kitasa wanaotaka kuua ukawa!
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema mipango inayofanywa...

Mbunge wa Nzega, Dr. Hamis kigwangalla asema hatowasusia fisi bucha!
Mbunge anayeshikilia jimbo la Nzega mjini, katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Dr. Hamis Kigwangalla, ametoa...

Wilaya ya Nzega
Wilaya ya Nzega ni miongoni mwa wilaya zinazounda mkoa wa Tabora, hapa Tanzania. Wilaya hii iko upande wa...

Prof. Peter Mutharika ametangazwa kuwa Rais nchini Malawi
Profesa Peter Mutharika aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu nchini Malawi kupitia chama cha...

Advertisement!

About this blog's Author!

Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as.....
Check him on Google+!

Advertisement!

No comments:

Post a Comment