Zanzibar, Tanzania, 04/07/2014. Wananchi wanaoishi katika visiwa vya Zanzibar wamelalamikia uhaba wa vituo vinavyouza umeme wa ZECO visiwani humo. Hayo tumeyashuhudia leo saa 2:00 usiku tulipotembelea kimoja kati ya vituo vitatu vikubwa kilichopo mtaa wa Kwa Mchina Mwanzo, mjini Unguja. Wananchi hao ambao walikuwa wamepanga foleni ndefu katika kituo hicho, walionyesha manung'uniko yao wakisema uhaba wa vituo vya ZECO (Zanzibar Electricity Corporation) unawafanya wapoteze muda mwingi wakisubiri huduma. Walisema vituo vyote vipo maeneo ya mjini na kwamba vyote vipo katika wilaya moja ya Mjini Magharibi, hali ambayo inamlazimu mwananchi anayeishi shamba kusafiri umbali mrefu kuja mjini kununua umeme. "....kwa mfano mtu kama mimi nimetoka zangu Mwera mpaka hapa, nimekuta foleni kubwa hali ilionitisha kiasi cha kutamani kurudi nyumbani, lakini itabidi nivumilie kwa sababu nisiponunua leo, kesho tena itanibidi nije hapa..." Alissema mmoja kati ya waliokuja kununua umeme ambaye alijitaja kwa jina la Ali. Uchache wa vituo vinavyotoa huduma za umeme wa ZECO limekuwa tatizo sugu kwa muda mrefu, na usumbufu wanaoupata wananchi sio kupanga foleni tu, bali pia umbali kutoka makwao. Vituo vikubwa vinavyofahamika zaidi ni pamoja na kile kilichopo maeneo ya Michenzani, Malindi na Kwa Mchina Mwanzo. Kwa upande mwingine, Timu ya Blog hii (mjknetten) iliyotia nanga katika kituo cha Kwa Mchina Mwanzo usiku huu saa 2:00, ilitaka kufahamu zaidi kuhusu chanzo cha foleni: Ni uhaba wa watoa huduma au idadi ya wateja ni kubwa kuliko uwezo wa vituo? Mwananchi mmoja ambaye hakutaka jina lake lifjulikane alijibu swali letu kwa ufasaha kabisa. "Ukisema uchache wa vituo ndio unaopelekea kuwepo kwa foleni kubwa, mi nitakataa, sio kweli. Mara ngapi mi nilishakuja hapa kununua umeme bila kukaa kwenye foleni. Kinachosababisha foleni leo hii ni mabadiliko ya ratiba zao za kazi kutokana na Mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Siku hizi vituo vinafunguliwa asubuhi saa 2 kama zamani. Saa 10 jioni vinafungwa kwa ajili ya wafanyakazi kwenda kufuturu, kisha vinafunguliwa tena saa 2 usiku baada ya watu kutoka Misikitini. Kwa hiyo vinapofungwa hiyo saa 10 mpaka saa 2, pana watu wengi wanaokuwa wameishiwa umeme, ndio maana ukienda michenzani au hapa kwa mchina, utakuta watu wengi...." Alisema mwananchi huyo. Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hemed mkazi wa maeneo ya Kiembe Samaki, alisema tatizo sio watoa huduma katika vituo hivyo kwenda kufuturu au kuswali, bali ni uchache au uhaba wa vituo. "Mimi nina imani kama vingelikuwepo vituo vingi, tusingerundikana katika kituo kimoja kama ilivyo sasa hivi, na watu tungepata huduma mapema na kuendelea na shughuli nyengine." Angalia Bongo watu wanavyopata umeme wa LUKU haraka, ni kwa sababu vituo vipo karibia kila mtaa, na vyengine sio vya serikali wala nini, ni wafanyabiashara wa uriani walioamua kuwasogezea raia wenzao huduma za umeme...." Aidha, msimamizi wa blog hii, Bw. Mpiga Kabeya, aliamua kuingia ndani ya jengo la kituo cha kwa Mchina Mwanzo kujionea hali halisi juu ya jinsi huduma zinavyotolewa. Kilichobainika ni kwamba, wafanyakazi wanajitahidi kutoa huduma kwa wateja kwa bidii kubwa. Kinachosababisha foleni ni uchache wa vituo, hali ambayo inapelekea mtu anayeishi maeneo ya mbali na vituo hivi kupata usumbufu. Watu wanaosafiri umbali mrefu kwenda katika maduka ya ZECO ni pamoja na wale wanaoishi mitaa ya Bububu, Fuoni, Jumbi, Kwanyanya, Uwanja wa Ndege, Masingini, Mwera, Chuini, Nungwi, Paje, Makunduchi, Kinuni, Amani, Daraja Bovu, Tunguu na maeneo mengine. Unaweza pia kupenda kusoma habari hizi hapa chini:
|
Internet basics tutorials! Learn the Internet basics on our free Internet tutorials. Learn how to surf the web and a variety of other related matters we offer on this blog. Get started now! Advertisement! Blogging tips and tutorials! Learn what the blog is, its importance, how to create it and other related topics in our free blogging tutorials! About this blog's Author!
Mpiga Kabeya is a Computer teacher. He also enjoys coding professionally, highly experienced on HTML, JavaScript, Php, Css, VB Script, etc. He is also a professional graphics designer as well as..... Advertisement! |
No comments:
Post a Comment